Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Aprili 6, 2018

Sipika job ndugai atoa ufafanuzi juu ya matibabu ya Tundu lisu

Picha
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai amesema utaratibu wa Bunge kugharamia matibabu ya Tundu Lissu unaendelea kufanyiwa kazi na ukikamilika utatolewa ufafanuzi. Spika Ndugai ametoa kauli hiyo Jana Alhamisi Aprili 5, 2018 wakati akihojiwa na Kituo cha Televisheni  hapa nchini ikiwa ni siku moja kupita tangu aliporejea nchini akitokea India kwa matibabu. Mhe Tundu Lissu ambaye ni mbunge wa Singida Mashariki kwa tiketi ya Chadema alishambuliwa kwa risasi zaidi ya 30, Septemba 7, 2017 na kupelekwa Hospitali ya Rufaa ya Dodoma na siku hiyohiyo alihamishiwa Hospitali ya Nairobi ambako alilazwa hadi Januari 6 alipohamishiwa Ubelgiji katika Hospitali ya Chuo Kikuu cha Leuven, anakoendelea na matibabu. Tangu wakati huo, familia yake na viongozi wa Chadema wamekuwa wakililalamikia Bunge kutogharamia matibabu ya mbunge huyo huku Lissu naye mara kadhaa akizungumzia jambo hilo. Lakini katika mahojiano hayo aliyofanya na mtangazaji wa televisheni hiyo, Charles Hilary...
Picha