Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Aprili 18, 2018

tanzania yawakumbuka wachina waliofariki ujenzi wa tazara.

Tanzania Yawakumbuka Wachina waliofariki ujenzi wa Tazara na kubainisha kutumia FOCAC kujitangaza Theopista Nsanzugwanko, DAR ES SALAAM USHIRIKIANO baina ya Tanzania na China ulianza siku nyingi wakati wa waasisi Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere na Mwenyekiti Mao Zedong wa China ambao umeendelea mpaka sasa kwa viongozi wan chi hici mbili  Rais John Magufuli na Rais Xi Jinping  wa China. Uhusiano huo unaoendelea katika masuala mbalimbali ya kiuchumi,kisiasa na kijamii ulinza miaka mingi kwa kuanzia na ujenzi wa reli ya Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (Tazara) iliyogeuka kuwa kichocheo kikubwa cha ukombozi kwa nchi za Kusini mwa Afrika. Wananchi wa China walikubali kutoa michango ya hali na mali ili kufanikisha ujenzi wa reli hiyo huku wakikabiliwa na ufukara wao na serikali yao na wameendelea kuwa marafiki wa kweli kwa Watanzania bila kuwageuka, hadi Taifa hilo lilipofanya mageuzi makubwa ya kiuchumi na kuwa moja ya nchi tajiri duniani. Mbali na hiyo, Mwalimu Nye...