sipoka ndungai apuuzia hoja ya kubenea.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Job Ndugai ameitupilia mbali hoja ya Mbunge wa Ubungo, Mhe Saed Kubenea (Chadema), kuhusiana na marekebisho ya masuala yanayohusu Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC). Akizungumza Jana bungeni mara baada ya kumalizika kwa kipindi cha maswali na majibu, ambapo alisema anaikataa taarifa ya mbunge huyo na akajipange upya. “Kwa hiyo taarifa yako Mhe Kubenea naikataa kwa hiyo kajipange tena, kama bado una nia uje katika utaratibu unaotakiwa kama hatukukuelewa tutatafuta muda ili tueleweshane zaidi ila sisi tumeelewa hivyo", alisema Spika Ndugai. “Mhe Saed Kubenea ameleta kusudio la kuwasilisha hoja binafsi bungeni akitaka Bunge lifanye marekebisho ya masuala yanayohusiana na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC)", alisema Spika Ndugai. "Ili ikidhi matakwa ya mfumo wa vyama vingi hapa nchini sasa kwa kuwa Tume hiyo ya Taifa ya Uchaguzi imeanzishwa na Katiba katika ibara ya 74 marekebisho yote juu ya tume...