RAIS AFANYA UTEUZI WA VIONGOZI ASUBUI HII
Asubuhi ya leo April 23, 2018, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, amefanya mabadiliko ya kiuongozi katika Benki ya Posta Tanzania (TPB). Rais Magufuli amemteua Dkt. Edmund Bernard Mndolwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Posta Tanzania (TPB), nafasi iliyokuwa ikishikiliwa na Prof. Lettice Rutashobya, ambae amemaliza muda wake. Kwa mujibu wa Ikulu, uteuzi wa Dkt. Edmund Bernard Mndolwa umeanza leo tarehe 23, April, 2018.