wasanii na wananchi wakiwa katka viwanya vya leaders kwaajili ya kumuaga MASOGANGE.
Wasanii mbalimbali na wakazi wa jiji la Dar es Salaam, wamejitokeza Leo katika Viwanja vya Leaders, jijini hapa, kwa ajili ya kumuaga msanii anayepamba video za wasanii ‘video queen’ Agnes Gerald, maarufu Masogange.
Mwili wa Masogange umewasili viwanjani hapa saa 11:24 asubuhi hii.
Msanii wa filamu na rafiki wa karibu wa marehemu, Irene Uwoya alibeba msalaba wakati mwili huo ukiingia Leaders.
Wasanii wengine walioonekana viwanjani hapo ni Mrisho Mpoto, Jackline Wolper, Chege, Timbulo, Kajala na Aunt Ezekiel. Wengine ni ‘video queen’ Tunda, msanii wa filamu, Rammy Ghalis.
Mshereheshaji katika shughuli hiyo leo ni MC Pilipili.
Masogange anatarajia kuzikwa kijijini kwao Utengule, Mbeya kesho.
Maoni
Chapisha Maoni