RAIS AMEFANYA UTEUZI WA MAJAJI.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli Leo Tarehe 15 Aprili 2018 amefanya uteuzi wa majaji 10 wa Mahakama kuu ya Tanzania, Naibu mwanasheria mkuu wa serikali (Deputy Attorney General-DAG), Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka (Deputy Director of public prosecutions- DDPP), Wakili Mkuu wa Serikali(Solicitor General) na Naibu Wakili Mkuu wa Serikali (Deputy Solicitor General). Walioteuliwa ni; (1) Bw Elvin Cloud Mugeta. (2) Bw Elinaza Benjamin Luvanda. (3) Bw Yose Joseph Mlyambina. (4) Bi Immaculata Kanjetan Banzi. (5) Bw Mustafa Siyani. (6) Bw Paul Joel Ngwembe. (7) Bi Agnes Zephania Mgeyekwa. (8) Bw Stephen Murimi Magaiga. (9) Bw Thadeo Mwenempazi. (10) Bi Butamo Kasuka Philip. Kabla ya uteuzi huu Bi But...