Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Aprili 10, 2018

MUGABE AKATAA KUTOA FUNGUO ZA IKURU

Picha
Rais wa zamani wa Zimbabwe, Robert Mugabe, bado anashikilia funguo rasmi za Ikulu zaidi ya miezi minne tangu alipolazimishwa kustaafu. George Charamba ambaye ni msemaji wa Rais Emmerson Mnangwagwa, aliliambia gazeti binafsi la Standard juzi; “Kuna mtu haiambii nchi kuwa rais wa zamani bado anashikilia funguo za Ikulu.” Kauli ya Charamba, inakuja baada ya madai kuwa laptop zilizohifadhiwa na mke wa rais huyo wa zamani, Grace Mugabe katika makontena yaliyopo Zimbabwe House, ambayo ni sehemu ya Ikulu mjini Harare, hazijulikani zilipo. “Mnangagwa hajatia mguu Zimbabwe House wala hamiliki funguo. Inakuaje uendelee kukaa na fungua ukifahamu nyumba ina wakazi wapya?” alisema na kuhoji Charamba ambaye awali alikuwa msemaji wa Mugabe. Mugabe (94) alilazimishwa kujiuzulu Novemba mwaka jana baada ya jeshi kuitwaa nchi kuzuia kile kilichoonekana kumrithisha madaraka mkewe Grace, ambaye alishinikiza kufukuzwa kwa Mnangagwa umakamu wa rais. Wiki iliyopita, gazeti binafsi ...