SASA MSAJILI WA VYAMA APATA NGUVU BUNGENI
Bunge limeiagiza Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, kutosita kufuta chama chochote cha siasa kinachokiuka sheria, kanuni na taratibu za uendeshaji wa vyama vya siasa. Hayo yalisemwa Jana bungeni mjini Dodoma na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria, Mhe Mohamed Mchengerwa, alipokuwa akisoma maoni ya kamati yake, kuhusu utekelezaji wa Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka 2018/19. “Kamati inashauri na kusisitiza kwamba Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa ihakikishe kunakuwepo na usimamizi wa karibu kwa kufuatilia na kuchunguza mienendo inayoharibu sifa na vigezo vya vyama vya siasa nchini", alisema Mhe Mchengerwa. “Na kwamba Msajili asisite kufuta usajili wa chama chochote cha siasa kitakachokiuka sheria, kanuni na taratibu za uendeshaji wa vyama vya siasa,” alisema Mchengerwa katika hotuba yake ya kamati aliyowasilisha bungeni", alisema Mhe Mchengerwa. Alisema pia kamati hiyo inaishauri ofisi hiyo ifanye ufuatiliaj...