Majambazi wavamia kanisa
Usiku wa kuamkia Leo Aprili 05, 2018 majambazi wamevunja Kanisa katoliki katika Parokia ya Mtakatifu Theresia, Mbezi Mwisho jijini Dar es Salaam na kupora sadaka na vikombe vitano vya misa.
Kwa maelezo yaliyotolewa na Padre wa Dekania ya Kibaha ya Kanisa Katoliki, Fr Benno Kikudo, amesema kuwa walinzi wa Parokia hiyo walipigwa na kuumizwa ila hawakuweza kuifikia nyumba ya mapadre.
“Usiku wa kuamkia leo, mapadre wenzetu wa parokia ya Mt. Theresia, Mbezi Mwisho waliingiliwa na majambazi kanisani. Majambazi walivunja mlango wa sakristia. Wameiba sadaka na vikombe vitano vya misa. Majambazi waliwapiga na kuwaumiza walinzi wa parokia. Bahati nzuri hawakuingia nyumba ya mapadre,” ameandika Fr Kikudo kwenye taarifa yake aliyoitoa leo kufuatia tukio hilo.
Tayari Kamanda wa polisi kanda maalumu ya Dar es salaam, Lazaro Mambosasa amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.
Maoni
Chapisha Maoni