mvua yasababisha mabsa bas ya mwendo kasi kusitisha huduma

Kampuni inayotoa huduma katika mradi wa mabasi yaendayo haraka (UDART) imeamua kusitisha usafirishaji wa abiria kwa baadhi ya njia kuanzia saa 11:00 alfajiri kutokana na kufungwa kwa barabara ya Morogoro eneo la Jangwani kutokana na mafuriko yaliyosababishwa na mvua zinazoendelea kunyesha

Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano UDART, Deus Bugaywa na kusema wamechukua maamuzi hayo kutokana na maji mengi ya mvua kupita juu ya daraja la Mto Msimbazi Jijini Dar es Salaam hali ambayo inahatarisha usalama wa abiria na vyombo vya usafirishaji.

"Kwa sasa huduma zinatolewa kwa njia za Kimara - Morroco, Kimara - Magomeni Mapipa, na Gerezani - Muhimbili. Huduma kamili zitarejea mara baada ya barabara kufunguliwa", amesema Bugaywa.

Kwa upande mwingine, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano UDART, Deus Bugaywa amewaomba radhi wananchi wanaotumia usafiri huo kwa usumbufu ambao umejitokeza.

Maoni

  1. Lucky Club Casino Site - Play with $10 Free on Lucky Club
    The Lucky Club luckyclub Casino will be the place where you can meet the people who love casino games and win real money. Our casino floor has over 1600 slots and video

    JibuFuta

Chapisha Maoni

HABARI

NANDY AOMBA MSAMAHA KUHUSU KUVUJA KWA VIDEO YAKE AKIFANYA MAPENZI NA BIL NAS

Nyimbo za singeri nchini zifungiwe na jita tz soma zaidi hapa...