RAIS AMEFANYA UTEUZI WA MAJAJI.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli Leo Tarehe 15 Aprili 2018 amefanya uteuzi wa majaji 10 wa Mahakama kuu ya Tanzania, Naibu mwanasheria mkuu wa serikali (Deputy Attorney General-DAG), Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka (Deputy Director of public prosecutions- DDPP), Wakili Mkuu wa Serikali(Solicitor General) na Naibu Wakili Mkuu wa Serikali (Deputy Solicitor General).
Walioteuliwa ni;
(1) Bw Elvin Cloud Mugeta.
(2) Bw Elinaza Benjamin Luvanda.
(3) Bw Yose Joseph Mlyambina.
(4) Bi Immaculata Kanjetan Banzi.
(5) Bw Mustafa Siyani.
(6) Bw Paul Joel Ngwembe.
(7) Bi Agnes Zephania Mgeyekwa.
(8) Bw Stephen Murimi Magaiga.
(9) Bw Thadeo Mwenempazi.
(10) Bi Butamo Kasuka Philip.
Kabla ya uteuzi huu Bi Butamo Kasuka Philip alikuwa Naibu katibu mkuu ofisi ya makamu wa Rais.
Aidha, Rais Magufuli amemteua Dkt Evaristo Emmanuel Hongopa kuwa Naibu mwanasheria mkuu wa serikali (DAG).
Dkt Hongopa amechukua nafasi ya Bw Paul Joel Ngwembe ambaye ameteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama kuu Tanzania.
Rais Magufuli amemteua Bw Edson Athanas Makallo kuwa Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka (Deputy Director of Public prosecutions).
Pia Rais Magufuli amemteua Dkt Julius kuwa Wakili Mkuu wa Serikali (Solicitor General).
Rais Magufuli amemteua Dkt Ally Possi kuwa Naibu Wakili Mkuu wa Serikali (Deputy Solicitor General).
Rais Magufuli amefafanua kuwa amefanya uteuzi huo wa majaji wa Mahakama kuu kwa lengo la kujaza nafasi za majaji waliostaafu na Rais Magufuli amefanya uteuzi wa Wakili Mkuu wa Serikali na Naibu Wakili Mkuu wa Serikali kwa lengo la kuhakikisha ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali, Mkurugenzi wa Mashtaka na Wakili Mkuu wa Serikali zinafanya kazi vizuri zaidi kushughulikia masuala ya Mahakama.
Maoni
Chapisha Maoni