sipoka ndungai apuuzia hoja ya kubenea.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Job Ndugai ameitupilia mbali hoja ya Mbunge wa Ubungo, Mhe Saed Kubenea (Chadema), kuhusiana na marekebisho ya masuala yanayohusu Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).
Akizungumza Jana bungeni mara baada ya kumalizika kwa kipindi cha maswali na majibu, ambapo alisema anaikataa taarifa ya mbunge huyo na akajipange upya.
“Kwa hiyo taarifa yako Mhe Kubenea naikataa kwa hiyo kajipange tena, kama bado una nia uje katika utaratibu unaotakiwa kama hatukukuelewa tutatafuta muda ili tueleweshane zaidi ila sisi tumeelewa hivyo", alisema Spika Ndugai.
“Mhe Saed Kubenea ameleta kusudio la kuwasilisha hoja binafsi bungeni akitaka Bunge lifanye marekebisho ya masuala yanayohusiana na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC)", alisema Spika Ndugai.
"Ili ikidhi matakwa ya mfumo wa vyama vingi hapa nchini sasa kwa kuwa Tume hiyo ya Taifa ya Uchaguzi imeanzishwa na Katiba katika ibara ya 74 marekebisho yote juu ya tume hiyo yanatakiwa kuletwa kwa kupitia muswada wa marekebisho ya Katiba na sio hoja binafsi ya mbunge,” alisema Spika Ndugai.
Pia Spika alisema katika alichokisema Mhe Kubenea ni jambo linalihusu Katiba ambapo kutokana na hali hiyo upo utaratibu wa kuafuata ili kuweza kuendana na mabadiliko hayo ya katiba ya nchi.
Pamoja na hali hiyo, Spika Ndugai, alisema wabunge wamekuwa na shida ya jinsi ya kuwasilisha hoja binafsi.
“Lakini pia tumekuwa na shida kidogo katika jambo hili kutuletea taarifa ofsini ya kwamba wanakusudia kuleta hoja binafsi halafu baadhi yao taarifa hiyo haijafika hata ofsini wameishaweka katika Mtandao", alisema Spik Ndugai.
“Hata Spika naanza kuisoma katika Mtandao na wanawachanganya wananchi kwa sababu hatua ni mbili,” alisema Spika Ndugai.
Spika Ndugai alisema hatua hizo ni pamoja na kuwasilisha taarifa kwa Katibu wa Bunge na baadae kuiwasilisha hoja yenyewe.
“Wengi wanaleta tu hoja mfano Mheshimiwa Bashe (Husein) na wengine inaweza kuwa ni mjadala wa kitaifa hivi na wananchi wengi wanaamini umepeleka hoja kumbe hakuna hoja,” alisema Spika Ndugai.
Maoni
Chapisha Maoni