Machapisho

Sipika job ndugai atoa ufafanuzi juu ya matibabu ya Tundu lisu

Picha
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai amesema utaratibu wa Bunge kugharamia matibabu ya Tundu Lissu unaendelea kufanyiwa kazi na ukikamilika utatolewa ufafanuzi. Spika Ndugai ametoa kauli hiyo Jana Alhamisi Aprili 5, 2018 wakati akihojiwa na Kituo cha Televisheni  hapa nchini ikiwa ni siku moja kupita tangu aliporejea nchini akitokea India kwa matibabu. Mhe Tundu Lissu ambaye ni mbunge wa Singida Mashariki kwa tiketi ya Chadema alishambuliwa kwa risasi zaidi ya 30, Septemba 7, 2017 na kupelekwa Hospitali ya Rufaa ya Dodoma na siku hiyohiyo alihamishiwa Hospitali ya Nairobi ambako alilazwa hadi Januari 6 alipohamishiwa Ubelgiji katika Hospitali ya Chuo Kikuu cha Leuven, anakoendelea na matibabu. Tangu wakati huo, familia yake na viongozi wa Chadema wamekuwa wakililalamikia Bunge kutogharamia matibabu ya mbunge huyo huku Lissu naye mara kadhaa akizungumzia jambo hilo. Lakini katika mahojiano hayo aliyofanya na mtangazaji wa televisheni hiyo, Charles Hilary...
Picha

SASA MSAJILI WA VYAMA APATA NGUVU BUNGENI

Picha
Bunge limeiagiza Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, kutosita kufuta chama chochote cha siasa kinachokiuka sheria, kanuni na taratibu za uendeshaji wa vyama vya siasa. Hayo yalisemwa Jana bungeni mjini  Dodoma  na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria, Mhe Mohamed Mchengerwa, alipokuwa akisoma maoni ya kamati yake, kuhusu utekelezaji wa Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka 2018/19. “Kamati inashauri na kusisitiza kwamba Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa ihakikishe kunakuwepo na usimamizi wa karibu kwa kufuatilia na kuchunguza mienendo inayoharibu sifa na vigezo vya vyama vya siasa nchini", alisema Mhe Mchengerwa.  “Na kwamba Msajili asisite kufuta usajili wa chama chochote cha siasa kitakachokiuka sheria, kanuni na taratibu za uendeshaji wa vyama vya siasa,” alisema Mchengerwa katika hotuba yake ya kamati aliyowasilisha bungeni", alisema Mhe Mchengerwa.  Alisema pia kamati hiyo inaishauri ofisi hiyo ifanye ufuatiliaj...

MBUNGE WA CHADEMA MAHAKAMIAN

Picha
Mbunge wa Tarime Vijijini, Mhe John Heche amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kusomewa mashtaka matatu yakiwamo kufanya uchochezi wa chuki kwa wananchi dhidi ya serikali. Mhe Heche amefikishwa mahakamani hapo leo Alhamisi aprili 5, 2018,  baada ya kujisalimisha polisi alikokua akishikiliwa tangu juzi. Akisomewa mashtaka hayo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri, Mhe Heche anadaiwa kutenda kosa hilo akiwa katika mkutano wa hadhara uliofanyika Viwanja vya Buibui Kinondoni, jijini Dar es Salaam Februari 16, mwaka huu. Katika mashtaka mengine, anadaiwa kufanya mkusanyiko pamoja usio halali pamoja na wenzake saba akiwamo Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Mhe Freeman Mbowe na kuendelea kukusanyika na kusababisha kifo cha mwanafunzi wa mwaka wa kwanza wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Aquilina Akwilini na askari kujeruhiwa. Mhe Heche ameunganishwa katika kesi inayowakabili viongozi wengine saba wa chama hicho waliopata dhaman ...

Majambazi wavamia kanisa

Picha
Usiku wa kuamkia Leo Aprili 05, 2018 majambazi wamevunja Kanisa katoliki katika Parokia ya Mtakatifu Theresia, Mbezi Mwisho jijini Dar es Salaam  na kupora sadaka na vikombe vitano vya misa. Kwa maelezo yaliyotolewa na Padre wa Dekania ya Kibaha ya Kanisa Katoliki, Fr Benno Kikudo, amesema kuwa walinzi wa Parokia hiyo walipigwa na kuumizwa ila hawakuweza kuifikia nyumba ya mapadre. “Usiku wa kuamkia leo, mapadre wenzetu wa parokia ya Mt. Theresia, Mbezi Mwisho waliingiliwa na majambazi kanisani. Majambazi walivunja mlango wa sakristia. Wameiba sadaka na vikombe vitano vya misa. Majambazi waliwapiga na kuwaumiza walinzi wa parokia. Bahati nzuri hawakuingia nyumba ya mapadre,” ameandika Fr Kikudo kwenye taarifa yake aliyoitoa leo kufuatia tukio hilo. Tayari Kamanda wa polisi kanda maalumu ya Dar es salaam, Lazaro Mambosasa amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.

JITA TZ GROUP

Picha
https://chat.whatsapp.com/5ju0hFjUzD3KGJLanyPztQ Sasa unaweza kujiunga kwenye grp la whatsapp kipitia link hiyo hapo juu☝☝☝

MAHAKAMANI

Mahakama imewaachia wangonjwa 55 wa akili.  >> http://kulunzifikra.blogspot.com/2018/03/mahakama-imewaachia-wangonjwa-55-wa.html