Machapisho

RAIS AFANYA UTEUZI WA VIONGOZI ASUBUI HII

Picha
Asubuhi ya leo April 23, 2018, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, amefanya mabadiliko ya kiuongozi katika Benki ya Posta Tanzania (TPB). Rais Magufuli amemteua Dkt. Edmund Bernard Mndolwa kuwa Mwenyekiti  wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Posta Tanzania (TPB), nafasi iliyokuwa ikishikiliwa na Prof. Lettice Rutashobya, ambae amemaliza muda wake. Kwa mujibu wa Ikulu, uteuzi wa Dkt. Edmund Bernard Mndolwa umeanza  leo tarehe 23, April, 2018.

MSIBANI DIAMOND AKISALIMIANA NA ALL KIBA KWA KUPEANA MIKONI

Picha
Wasanii maarufu wa muziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz na Ali Kiba wamekutana katika msiba wa Agnes Masogange na kusalimiana. Mara baada ya wasanii hao kusalimiana kwa kupeana mikono wakiwa katika meza kuu, waombolezaji waliojaa kwenye Viwanja vya Leaders walipiga kelele. Diamond alimsalimia Kiba kwa kumpa mkono, kisha wawili hao walikumbatiana na baada ya tukio hilo, MC Pilipili alisikika akisema: “Unaona sasa, hawana ugomvi hawa.” Kumekuwa na taarifa za wanamuziki hao kuwa na ugomvi kwa muda mrefu ambao hata hivyo, unatajwa kutengenezwa na mashabiki wao wa ‘Team Kiba na Team Diamond.’ Akizungumzia katika viwanja hivyo, Ali Kiba ambaye ametoka kuchukua jiko hivi karibuni, amesema harusi na kifo vyote ni ibada na ndiyo maana amefika kuungana na waombolezaji wengine ingawa bado yupo fungate. Masogange alifariki dunia juzi katika Hospitali ya Mama Ngoma, Mwenge ambako alilazwa kwa siku nne.

wasanii na wananchi wakiwa katka viwanya vya leaders kwaajili ya kumuaga MASOGANGE.

Picha
Wasanii mbalimbali na wakazi wa jiji la Dar es Salaam, wamejitokeza Leo katika Viwanja vya Leaders, jijini hapa, kwa ajili ya kumuaga msanii anayepamba video za wasanii ‘video queen’ Agnes Gerald, maarufu Masogange. Mwili wa Masogange umewasili viwanjani hapa saa 11:24 asubuhi hii. Msanii wa filamu na rafiki wa karibu wa marehemu, Irene Uwoya alibeba msalaba wakati mwili huo ukiingia Leaders. Wasanii wengine walioonekana viwanjani hapo ni Mrisho Mpoto, Jackline Wolper, Chege, Timbulo, Kajala na Aunt Ezekiel.  Wengine ni ‘video queen’ Tunda, msanii wa filamu, Rammy Ghalis. Mshereheshaji katika shughuli hiyo leo ni MC Pilipili. Masogange anatarajia kuzikwa kijijini kwao Utengule, Mbeya kesho.

follow and join on whatsApp group

Picha
Follow this link to join my WhatsApp group: https://chat.whatsapp.com/Hngu3JSEx7P9dThWlRsE3A

BREAKING NEWS; R.I.P AGNESS MASOGANGE (THE VIDEO VIXEN IN TANZANIA DIED TODAY AFTERNOON).

Picha
The video vixen in Tanzania who is famous as AGNESS MASOGANGE has died, the news from his nearly person stated that masogange died to day afternoon. but until now there are no any report about the cause of her death. official mapato tv, is trying to search more information about the death of the this video vixen in tanzania. agness masogange is the famous in different bongo videos where she acted in different movies and also participated in different music video as a video queen. ones we get the full information about he death we shall post it in this site. so you can submit you email by filling the boxes bellow so as we can email you when we will provides this information or news and many other  trending news and hot entertainments

tanzania yawakumbuka wachina waliofariki ujenzi wa tazara.

Tanzania Yawakumbuka Wachina waliofariki ujenzi wa Tazara na kubainisha kutumia FOCAC kujitangaza Theopista Nsanzugwanko, DAR ES SALAAM USHIRIKIANO baina ya Tanzania na China ulianza siku nyingi wakati wa waasisi Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere na Mwenyekiti Mao Zedong wa China ambao umeendelea mpaka sasa kwa viongozi wan chi hici mbili  Rais John Magufuli na Rais Xi Jinping  wa China. Uhusiano huo unaoendelea katika masuala mbalimbali ya kiuchumi,kisiasa na kijamii ulinza miaka mingi kwa kuanzia na ujenzi wa reli ya Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (Tazara) iliyogeuka kuwa kichocheo kikubwa cha ukombozi kwa nchi za Kusini mwa Afrika. Wananchi wa China walikubali kutoa michango ya hali na mali ili kufanikisha ujenzi wa reli hiyo huku wakikabiliwa na ufukara wao na serikali yao na wameendelea kuwa marafiki wa kweli kwa Watanzania bila kuwageuka, hadi Taifa hilo lilipofanya mageuzi makubwa ya kiuchumi na kuwa moja ya nchi tajiri duniani. Mbali na hiyo, Mwalimu Nye...

mbowe amtelekeza TUNDU LISU uberigiji

Picha
*MBOWE AMTELEKEZA LISSU UBELGIJI* . By JITATZ- April 16, 20180140 . –#Wabunge Saed Kubenea, Anthony Komu wawa chanzo cha mateso ya mwenzao -#Awasusia wamhudumie kwa kusema wameingilia kati mgonjwa wake -#Atangaza kumsusa na kuiagiza kamati kuu yake isijihusishe naye kwa lolote -#Amehifadhiwa Ubelgiji kwa Mtanzania anayeishi huko, nyumba moja ya vyumba viwili na sebule anaishi Lissu, mke wake na watu wengine saba – #Anaishi maisha magumu ya mateso na fedheha kubwa asiyowahi kuyafikiria huku akienda hospitali na kurudi -#Wabunge, wanachama wagawanyika wakimshangaa Mbowe kuzuia mabilioni ya chama kumsaidia kiongozi wao muhimu –#Chama kinapokea Bilioni 4.5 za ruzuku kila mwaka, milioni 680 ya michango ya wabunge kila mwaka lakini kimemtelekeza mbunge wake Na Shaaban Ismail HALI ya huduma za kimatibabu na maisha kwa jumla ya Mbunge wa Singida Mashariki (CHADEMA), Tundu Lissu, nchini Ubelgiji, zimezidi kuwa ngumu na sasa mbunge huyo anaishi kwa msaada wa wasamari...