SABABU ZA KUSHINDWA KWA MAANDAMANO

*SABABU ZA KUSHINDWA KWA MAANDAMANO YA MBOWE KUPITIA  MANGE*.

Imeandikwa na;
*Philipo Mwakibinga*
26/04/2018.

Kwanza nitoe niweke wazi  kuwa mimi ni mzoefu na nguli wa maandamano na jamii ninayoishi nayo inajua hivyo.

Nilianza kuandamana kabla hata Mange hafikiri wala kutamani kuandamana, kipindi mimi naandamana na kuongoza maandamano ambayo yalikuwa yanaungwa mkono na yalileta tija, Mange alikuwa miongoni mwa wanaopinga na kubeza maandamano.

Kwa kua alikuwa upande wa waliochukizwa na maandamano nidhahili kuwa  Mange alikuwa hajawahi kabisa kuamini au kuota kama angetamani sikumoja kuandamana, hali hii ilimfanya ashindwe hata kujifunza au kupata nafasi ya kuelimishwa au kujielimisha juu ya maamdamano.

Mange kajikuta  anatumia nguvu nyingi kuandaa maandamano hewa.

Ni maandamano hewa kwasababu kashindwa na hatokuja kurudia tena kuamini kuwa anaweza kuandamanisha Watanzania.

*Kwasababu zifuatazo Mange kashindwa;*

*1*.Mange kwa dhamira yake ya dhati hana sababu ya msingi ambayo hata yeye inamgusa hata akaanzisha hayo maandamano ndiyo maana wanaomshabikia niwale wenye uelewa mdogo juu ya masuala ya kiuongozi na kisiasa, niwale mashabiki yaani bendera fuata upepo. Mange anapowajaza ujinga nao wanamjaza ujinga harafu siku inapofika kila mmoja ananunua mb na kujaza charge katika simu yake ili aone kupitia mitandao kama mwenzie kaenda kuandamana au laa!.

Ndiyo maana hata wale waliosema wameandamana nje ya Tanzania wengi mmewaona kama wasiojielewa na wasio na uhakika na wanachokifanya. Hawakua hata na sura za kuandamana na wengine walificha sura zao kwakua hawakua na dhamira. Mange unashindwa kwasababu wanaokutumia hawajakueleza kiundani wanachotaka ila wanachofanya ni kukuahidi ulinzi tu.

*2*. Watanzania hawaamini kuwa maandamano ndiyo njia ya kwanza ya kudai haki kama Mange anavyoamini.

*3*.Watanzania huwa wanataka sababu ya kuandamana iwe yenye tija na yenyekufafanulika na kueleweka kwa kila mtu.

*4*. Watanzania siyo waumini wa vyama vya siasa kwa kiwango cha fikra za Mange kwasababu walikuwepo hata kabla ya vyama vya siasa na hawajawai kuamini kuwa vyama vya siasa ndiyo kimbilio lao wanapopata matatizo au sintofahamu bali,wao  hukimbilia Utanzania wao wapatapo matatizo au masumbufu.

*5*.Watanzania wamekua sehemu ya masuluhisho na wasuluhishi wa migogoro mingi barani Afrika na kwa uzoefu huo wanajua vyanzo na matokeo ya migogoro mingi hivyo, wamejiandaa kuwa suluhu ya matatizo na si vyanzo vya matatizo.

Mfano idadi ya wakimbizi wanaoingia Tanzania ni elimu tosha kwa unaowategemea wakuungemkono.

*6*.Umbali aliopo kiongozi wa maandamano dhidi ya anaotaka waandamane nalo ni tatizo la karne.

Maandamano ya kutumia rimoti Watanzania hawajazoea, wanahitaji wamuone huyo anayewaongoza na waone naye anavyopata athari za moja kwamoja kuliko yeye kuwa sehemu ya nyama na asali wakati wao wapo kwenye maumivu makali.

*7* Mbowe hajawahi kuwa muandamanaji. Kila anaposhawishi kuandamana yeye hukimbia na kuelekea mbali zaidi na hata nje ya nchi. Viongozi wenzie hubaki wakitaabika na wananchi kuumizwa.

Ndiyo maana siku moja kabla ya leo aliandika barua ya kupinga maandamano hata bila kushirikisha chama chake ili kujiweka salama na kukuacha unahaha na kukosa ushirikiano.

Mwisho;
*Mange, Mbowe na mabeberu wanao watuma , KIMYA CHA MNAODHANI ADUI ZENU NI, HATARI KULIKO KELELE ZENU*

Maoni

HABARI

mvua yasababisha mabsa bas ya mwendo kasi kusitisha huduma

NANDY AOMBA MSAMAHA KUHUSU KUVUJA KWA VIDEO YAKE AKIFANYA MAPENZI NA BIL NAS

Nyimbo za singeri nchini zifungiwe na jita tz soma zaidi hapa...