TUNDU LISU KURUDI KUTOKA UBELIGIJI.

MBUNGE wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu aliyelazwanchini Ubelgiji anatarajiwakurudi nyumbani siku yoyote kuanzia juzi, baada ya madaktari kumaliza kumpatia matibabu,amesema.

Lissu ambaye amekuwa hospitalini tangu Septemba 7, mwaka janaaliposhambuliwa nyumbani kwake Area D, mjiniDodoma, aliliambia shirika la utangazaji la BBC juzi, kuwa kwa sasa hana tena kidonda cha risasi na yupo tayari kurudi nyumbani.

"Sina tena kidonda cha risasi, nilipigwa mara 16," alidai Lissu (50) nakufafanua "sina tena kiungo kilichovunjwa". "Nilikuwa nimevunjwamguu mmoja mara tatu, mikono yote ilikuwa imevunjwa, nilikuwa na risasi nyingi mwilini, na vidonda vingi."

Lissu ambaye pia ni Mnadhimu Mkuu wa Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni, alisema viungo vyotevilivyokuwa vimevunjika vimeshaunga. Alisema tangu aanze kupatamatibabu amefanyiwa operesheni 17, nne zikiwa sehemu ya tumbo, lakinisasa hali yake ni nzuri.

Lissu alisema analazimika kurundi nchini kwa kuwa yeye ni Mbunge, Kiongoziwa Upinzani Bungeni naWaziri kivuli wa Sheria na Katiba. Alisema kwa majukumu hayo hawezi kwenda mafichoni. "Siwezi kwenda mafichoni, siwezi kuikimbia nchi yangu,nitarudi Tanzania," alisema. "Mimi ni mbunge, mimi ni kiongozi bungeni, ni Mnadhimu Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani bungeni, mimi ni msemajiwa sheria na katiba wa chama changu."

Hata hivyo, akizungumza na Nipashe jana kaka wa Lissu, wakili Alute Mughwai alisema familia bado haijapokea taarifa ya siku anayotarajia kurudi. Alisema familiainachofahamu ni kuwa Lissu amefanyiwaoperesheni ya 19 wiki chache zilizopita, hivyo kutakuwa na uangalizi wa afya yake.
“Hayo mahojiano aliyofanya juzi sijayaona, nitawasiliana naye leo jioni (jana) nimsikilize, lakini sisi kama familia hatujapata taarifa yoyote lini atarudi, wala hatuwezi kujua haditupewe taarifa na hospitali,” alisema wakiliMughwai.

Lissu alipoulizwa na BBCendapo amepata msaadawa matibabu kutokaserikalini, alisema chombo pekee chenye wajibu wa kumgharamia matibabuyake ni Bunge na "siyoserikali, wala Ikulu, walamtu yoyote."

Source: Nipashe April 30, 2018

Maoni

  1. Best Casino Games in Virginia | Dr.MD.com
    Best casino games 경산 출장마사지 in Virginia - Play at the 사천 출장마사지 best online 공주 출장마사지 casinos, learn about the best online 공주 출장마사지 casino games, and 화성 출장안마 claim your bonuses. Rating: 4 · ‎1 vote

    JibuFuta

Chapisha Maoni

HABARI

mvua yasababisha mabsa bas ya mwendo kasi kusitisha huduma

NANDY AOMBA MSAMAHA KUHUSU KUVUJA KWA VIDEO YAKE AKIFANYA MAPENZI NA BIL NAS

Nyimbo za singeri nchini zifungiwe na jita tz soma zaidi hapa...