Machapisho

RAIS AMEFANYA UTEUZI WA MAJAJI.

Picha
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli Leo Tarehe 15 Aprili 2018 amefanya uteuzi wa majaji 10 wa Mahakama kuu ya Tanzania, Naibu mwanasheria mkuu wa serikali (Deputy Attorney General-DAG), Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka (Deputy Director of public prosecutions- DDPP), Wakili Mkuu wa Serikali(Solicitor General) na Naibu Wakili Mkuu wa Serikali (Deputy Solicitor General).                  Walioteuliwa ni;     (1) Bw Elvin Cloud Mugeta.       (2) Bw Elinaza Benjamin Luvanda.    (3) Bw Yose Joseph Mlyambina.    (4) Bi Immaculata Kanjetan Banzi.    (5) Bw Mustafa Siyani.    (6) Bw Paul  Joel Ngwembe.    (7) Bi Agnes Zephania Mgeyekwa.      (8) Bw Stephen Murimi Magaiga.    (9) Bw Thadeo Mwenempazi.   (10) Bi Butamo Kasuka Philip. Kabla ya uteuzi huu Bi But...

mvua yasababisha mabsa bas ya mwendo kasi kusitisha huduma

Picha
Kampuni inayotoa huduma katika mradi wa mabasi yaendayo haraka (UDART) imeamua kusitisha usafirishaji wa abiria kwa baadhi ya njia kuanzia saa 11:00 alfajiri kutokana na kufungwa kwa barabara ya Morogoro eneo la Jangwani kutokana na mafuriko yaliyosababishwa na mvua zinazoendelea kunyesha Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano UDART, Deus Bugaywa na kusema wamechukua maamuzi hayo kutokana na maji mengi ya mvua kupita juu ya daraja la Mto Msimbazi Jijini Dar es Salaam hali ambayo inahatarisha usalama wa abiria na vyombo vya usafirishaji. "Kwa sasa huduma zinatolewa kwa njia za Kimara - Morroco, Kimara - Magomeni Mapipa, na Gerezani - Muhimbili. Huduma kamili zitarejea mara baada ya barabara kufunguliwa", amesema Bugaywa. Kwa upande mwingine, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano UDART, Deus Bugaywa amewaomba radhi wananchi wanaotumia usafiri huo kwa usumbufu ambao umejitokeza.

tundu lisu atoa ujumbe kwa wanachama wa (TLC)

Picha
Wakati wajumbe wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) hii leo wakitarajia kumchagua rais wao, mmoja wa wagombea wa kiti hicho Wakili Fatma Karume anatazamwa kubeba kivuli cha kiongozi aliyemaliza muda wake, Tundu Lissu. Mazingira ya Fatma kubeba kivuli cha Lissu katika uchaguzi huo yamejionyesha wazi kutokana na mamia ya wanachama wa TLS wanaomuunga mkono Lissu, kuonyesha dhamira ya kumpigia kura. Jana Rais anayemaliza muda wake, Tundu Lissu alipata wasaa kuzungumza na mawakili wenzake hao waliokushanyika Arusha kupitia tamko lake lenye maneno 4096 alilolitoa kwa maandishi kutoka Ubelgiji anakoendelea na matibabu. Lissu licha ya wakuwashukuru wanataaluma wenzake kwa kushirikiana na wasamaria wema wengine kumsaidia kutokana na matatizo aliyoyapata, aliwakumbusha mawakili hao kwamba wakati wanapiga kura leo watambue kwamba wapo wenzao ambao wamekumbwa na madhira mbalimbali kama ilivyo kwa wananchi wengine ikiwamo kuwekwa ndani na kwamba uhuru uko shakani kwa kila mmoja kuanzia kw...

sipoka ndungai apuuzia hoja ya kubenea.

Picha
Spika  wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe  Job Ndugai ameitupilia mbali hoja ya Mbunge wa Ubungo, Mhe  Saed Kubenea (Chadema), kuhusiana na marekebisho ya masuala yanayohusu Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC). Akizungumza Jana bungeni mara baada ya kumalizika kwa kipindi cha maswali na majibu, ambapo alisema anaikataa taarifa ya mbunge huyo na akajipange upya. “Kwa hiyo taarifa yako Mhe Kubenea naikataa kwa hiyo kajipange tena, kama bado una nia uje katika utaratibu unaotakiwa kama hatukukuelewa tutatafuta muda ili tueleweshane zaidi ila sisi tumeelewa hivyo",  alisema Spika Ndugai.  “Mhe Saed Kubenea ameleta kusudio la kuwasilisha hoja binafsi bungeni akitaka Bunge lifanye marekebisho ya masuala yanayohusiana na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC)", alisema Spika Ndugai. "Ili ikidhi matakwa ya mfumo wa vyama vingi hapa nchini sasa kwa kuwa Tume hiyo ya Taifa ya Uchaguzi imeanzishwa na Katiba katika ibara ya 74 marekebisho yote juu ya tume...

serikali umetoa sababu za kukatika kwa umeme nchini

Picha
Serikali ya awamu ya tano kupitia Wizara ya Nishati imefunguka na kudai kukatika kwa umeme mara kwa mara kunatokana na sababu nyingi na wala sio kutokuwepo kwa umeme au miundo mbinu pekee yake kama baadhi ya wananchi wanavyokuwa wanafikilia. Hayo yamebainishwa na Waziri wa Wizara hiyo, Dkt Medard Kalemani leo Aprili kwenye kikao cha tisa mkutano wa 11 wa Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambalo linaendelea kufanyika Jijini Dodoma, wakati akijibu swali la Mbunge Temeke (CUF), Mh. Abdallah Mtolea aliyetaka kujua sababu zinazopelekea kukatika kwa umeme jiji la Dar es Salaam kwa ujumla mara kwa mara.  "Kukatika kwa umeme kuna tokana na sababu nyingi, siyo kwa sababu ya kutokuwepo kwa umeme au miundombinu. Wakati mwingine ni kasoro ndogo ndogo, tunakiri kabisa zipo changamoto za maeneo machache za kukatika kwa umeme kwenye baadhi ya nyakati za muda. Tunachokiomba ni kutupa taarifa inapotokea hitilafu ya namna hiyo", amesema Dkt Kalemani. Kwa upande mwingine, Dkt  K...

NANDY AOMBA MSAMAHA KUHUSU KUVUJA KWA VIDEO YAKE AKIFANYA MAPENZI NA BIL NAS

Picha
Nimesikitika sana, hiyo video ni ya ukweli ni ya mwaka 2016, nilikuwa na mahusiano na Bill Nas na tulikubaliana iwe siri, sasa sielewi kwa sababu gani kaamua kuvujisha, nimesikitishwa sana, ni video ambayo ilishutiwa kwa snapchat, sasa sielewi wakati ameipata hiyo video alikuwa nayo au alichukua mwenyewe, sijui niseme nini, naomba radhi sana kwa familia yangu, kanisani kwangu, serikali yangu, mashabiki, naomba radhi sana, adhabu ya maumivu ambayo nayapata imetokana na kumuamini mtu, ilikuwa ni private” :- Nandy Unamshauri nini Nandy kwa jambo hili

MUGABE AKATAA KUTOA FUNGUO ZA IKURU

Picha
Rais wa zamani wa Zimbabwe, Robert Mugabe, bado anashikilia funguo rasmi za Ikulu zaidi ya miezi minne tangu alipolazimishwa kustaafu. George Charamba ambaye ni msemaji wa Rais Emmerson Mnangwagwa, aliliambia gazeti binafsi la Standard juzi; “Kuna mtu haiambii nchi kuwa rais wa zamani bado anashikilia funguo za Ikulu.” Kauli ya Charamba, inakuja baada ya madai kuwa laptop zilizohifadhiwa na mke wa rais huyo wa zamani, Grace Mugabe katika makontena yaliyopo Zimbabwe House, ambayo ni sehemu ya Ikulu mjini Harare, hazijulikani zilipo. “Mnangagwa hajatia mguu Zimbabwe House wala hamiliki funguo. Inakuaje uendelee kukaa na fungua ukifahamu nyumba ina wakazi wapya?” alisema na kuhoji Charamba ambaye awali alikuwa msemaji wa Mugabe. Mugabe (94) alilazimishwa kujiuzulu Novemba mwaka jana baada ya jeshi kuitwaa nchi kuzuia kile kilichoonekana kumrithisha madaraka mkewe Grace, ambaye alishinikiza kufukuzwa kwa Mnangagwa umakamu wa rais. Wiki iliyopita, gazeti binafsi ...